Kongamano kitaifa la walimu Kiswahili shule za upili nchini 3/2/2024

Kongamano kitaifa la walimu Kiswahili shule za upili nchini 3/2/2024

MINT: KONGAMANO LA KITAIFA LA WALIMU WA KISWAHILI WA SHULE ZA UPILI NCHINI KENYA JUMAMOSI TARE 3 FEBRUARI 2024

Kwa mara nyingine idara ya Kiswahili ya shule ya upili ya Nakuru ikishirikiana na Kampuni ya Uchapishaji ya East African Educational Publishers (EAEP) wana fahari kuwaalika walimu wapendwa wa lugha ashirafu ya Kiswahili litakalofanyika katika ukumbi wa shule ya kitaifa ya Nakuru siku ya Jumamosi tarehe 3 Februari, 2024 kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa ku,i alasiri,

Kikako kitashughulikia mambo yafuatayo

1) Kanuni mpya na masuala ibuka utahini wa karatasi zote tatu za Kiswahili.

2) Namna ya kuwaandaa watahiniwa na kupata matokeo bora katika somo la Kiswahili.

3) Vitabu vipya vya Fasihi (Nguvu za Jadi, Bembea ya Maisha na Mapambazuko ya Machweo na Hadithi Nyingine).

Tumewaalika watahini wazoefu wa karatasi zote tatu za Kiswahili ambao walihusika katika usimamizi na usahihishaji wa KCSE 2023 na wana tajriba ya juu na ndefu katika ufundishaji, utahini na uandishi wa vitabu vya kiada, miongozo, vitabu vya marudio na marejeleo katika viwango vya shule za upili.

Aidha Mkurugenzi wa Elimu, Kaunti ya Nakuru atafungua rasmi warsha hii saa tatu Asubuhi.

Kila mwalimu mshiriki anaombwa kujisajili kwa kulipa Shilingi elfu mbili (Kshs 2000) siku hiyo.

Pesa hizo zitagharamia maandalizi, vyeti na shughuli nyinginezo. Kila mshiriki atapewa vitabu viwili vya Kiswahili.

Tafadhali thibitisha ushiriki wenu kabla ya tarehe 2/2/2024 ili maandalizi ya kufana yaafikiwe kupitia kwa nambari hii ya rununu 0728596680 Mzalendo Tomkim Baraza (Mwandalizi).

Wako Mwaminifu,
Mzalendo Tomkim Baraza
Simu 0728596680

error: Content is protected !!